MFAHAMU MSICHANA WA KIAFRIKA ALIYENYAYASIKA KWA AJILI YA KUWA NA UMBO ZURI LA KUVUTIA(SARAH BAARTIMAN) Na: IDRISA KITABUGE
Sarah Saartijie Baartiman ni mwanamke aliyezaliwa mwaka 1789 katika bonde Gamtoos mashariki mwa Afrika ya kusini. Alikuwa ni binti wa jamii ya watu wa KHOIKHOI ambao walikuwa maarufu sana kwasababu ya kuwa na makalio makubwa sana.  Kutokana na Sarah kujaaliwa umbo la kuvutia kwa kuumbwa vzuri na mwenyezi mungu. wazungu waliamuwa kumtumia kama chombo cha utalii na starehee. Wazungu walikuwa wakimuita HOTTENTOT VENUS ingawa kwa sasa ukilitumia hilo jina kumuita mtu huko Afrika kusini ni sawa na kumtusi na haliruhusiwi kutamkwa katika jamii ya watu wa khoi. Mwanamke huyu alijaliwa mwili mkubwa, sura nzuri na kila sifa za mwanamke wa kibantu aliyejaaliwa. Kutokana na hila za wazungu katika kipindi hicho cha ubaguzi wa kutisha. Sarah alienda uingereza na mwajiri wake aliyekuwa ni mtu mweusi aitwaye Hendrik cesars pamoja na daktari wa kizungu aitwaye william Dunlop aliyekuwa anafanya kazi kwenye kambi ya watumwa afrika kusini. Wakati wakiwa Afrika ya kusini kabla ya kwenda uingereza. Sarah, mwajiri wake na yule daktari wa kizungu walikubaliana kuwa wakienda huko uingireza wangemfanya kama maonesho kwa fedha, kwani Cesars alikuwa na deni kubwa kutoka kwa Dunlop na hivyo alimshawishi sarah(mfanya kazi wake) akubali ingawa mwazoni aligoma ila baadae alikubali.kwa sharti kuwa Caesars lazima waongozane naye kwenda huko uingereza. Walipofika huko uingereza alifanya maonyesho kwa takribani miaka minne na pia alifanya maonyesho na Ireland, ndani ya hiyo miaka minne alikuwa kivutio kikubwa kwa wazungu kuliko walivyotegemea kwani siku ya shoo yake watu walikuwa wanajaa sana na ikapelekea kulazimishwa kufanya maonyesho zaidi bila hiari yake kwani tyari walienda nje ya mkataba na Cesar's ilimuuma Sana na akaamua aondoke kurudi Afrika kusini na kumwacha Dunlop aendelee naye kwenye maonyesho bila ridhaa ya Sarah mwenyewe kukubali..... Picha namba (3) ni tangazo la kipindi hicho kuwa Sara atakuwepo sehemu Fulani kwa maonyesho. Ilipofika mwaka 1814 Dunlop alifariki na kuna mtu mmoja aitwaye henry Taylor aliaamua kumpeleka nchini ufaransa katika mji wa Paris na kumuuza kwa mkufunzi wa wanyama aitwaye S. Reaux ambaye naye alimpeleka kwa profesa mtafiti wa mambo ya kiihistoria, wanyama na mimiea aitwaye Georges Cuvier.  Huyu professa aliamua kufanya uchunguzi kupitia mwili wa sarah kuhusu kukosekana muunganiko kati ya wanyama na binadamu. (Dharau iliyoje). Na baada ya hapo aliendelea na maonyesho ambapo alifanyiwa unyama wa kutisha wa kila aina kutokana na kosa la kupewa umbo zuri na Mungu Mnamao tarehe 29/12/1815, mwanamke huyu akiwa bado binti mchanga aliaga dunia kifo chake kilisabishwa na mateso makali ya wazungu, waliokuwa wanamuingilia kimwili kwa idadi kubwa isio na mfano, kumsimamisha mrembo huyu kwa muda mrefu ili watu waweze kuona umbo lake hasa makalio yake kama chanzo cha wazungu kujipatia kipato. Lakini pia kuna vyanzo vingine vinasema pia aliugua ugonjwa wa kaswende. Haikuishia hapo Saartijie alipokwisha fariki mwili wake ulikaushwa na kuhifadhiwa makumbusho nchini ufaransa ili kuja kuwa kivutio cha utalii kwa vizazi vijavyo. Baada ya kufariki raia wa Afrika Kusini hasa weusi walikuwa wanaishinikiza Serikali ya Ufaransa kuwapa mwili wa mwanamke huyo ili wamzike kiheshima, na mnamo mwaka 2002 mwili wa Sarah ulizikwa tena mjini Pretoria nchini Afrika Kusini, ilitokana na Juhudi Kubwa zilizofaywa na Rais Nelson Mandela na raia wa Afrika Kusini.  Ukisoma vzuri unapata kuona ni jinsi gani Dada zetu wa kiafrika walivyokuwa wananyanyasika sana, inasikitisha sana na inauma mno... Wazungu hawakuwa na huruma wala upendo kabixa na sisi...!!! Picha namba (3) ndo sehemu aliyozikwa Sarah baada ya kurudishwa kutoka ufaransa...!!!! MWISHO...!!!